Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Subhani aliithamini siku ya ujenzi wa Msikiti wa Jamkarani.
Maelezo ya ujumbe wake ni kama ifuatavyo:
Bismillah al-Rahman al-Rahim
Mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni mwezi wa kushuka rehema za Mwenyezi Mungu, baraka zisizo hesabika na msamaha wa dhambi.
Kwa mujibu wa nukuhu, Msikiti wa Jamkaran ulijengwa mnamo tareh 17 Ramadhani mwaka 373 Hijria, kwa mwongozo wa Imam Al-Zaman (a.j), na leo hii mahali hapa ni Qabah ya mioyo ya wapenzi wa wilaya na wenye kusubiri kudhihiri kwa alie hoja ya mwisho ya Mwenyezimungu.
Bila shaka, mahali hapa takatifu ni ishara ya muungano wa kina wa waumini na Imam Al-Zaman (a.s), na ni fursa ya kipekee kwa wapenzi wa Imam huyo katika faragha kumuomba Mwenyezi Mungu kwa moyo uliojaa upendo na matumaini, na kutaka kuharakishwa kudhihiri kwake.
Ni uzuri ulioje katika usiku hu wa Qadr na katika sehemu hii, tuielekeze mikono yetu kwa Mwenyezi Mungu, tukimuomba heshima na utukufu kwa Waislamu wote, kuangamizwa maadui wa Uislamu, na kuondoa uovu wa maadui wa dini.
Ja'far Subhani
Maoni yako